DKT. BITEKO ATOA POLE KWA MASAUNI

 Na mwandishi wetu

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amejumuika na Wananchi wa Zanzibar pamoja na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Swala na Mazishi ya Baba Mzazi wa Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mzee Masauni Yussuf Masauni ambaye alikuwa Afisa Uhamiaji Mkuu Mstaafu Zanzibar.


Swala imefanyika msikiti wa Kilimani na kuzikwa kwenye Makaburi ya Mwanakwerekwe, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Zanzibar Tarehe 24/02/2024.


Inna liilahi wainna ilaihi raajiun
Post a Comment

0 Comments