KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI MRADI WA BOOST SHULE YA IGIMA

 Na. Asila Twaha, Mlimba


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imeridhishwa na  utekelezaji wa ujenzi wa shule ya Msingi Igima unaotekelezwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kupitia Mradi wa Kuboresha Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) katika Wilaya ya Mlimba mkoani Morogoro.


Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Denis Londo akizungumza Februari 21 2024 kwenye ya kamati hiyo ya kukagua miradi ya elimu wilayani humo,  amesema kila mtu akiwajibika katika nafasi yake akifanya kazi nzuri kwa weledi   anaisaidia Serikali lakini pia mradi umeonesha  kukidhi viwango  na thamani ya fedha iliyotolewa.


"Kamati imeridhishwa na uongozi wa shule ya msingi Igima kwa jinsi mlivyowajibika katika usimamizi wa mradi huu ni watie moyo endeleeni kufanya kazi ili kwa pamoja tuwatumikie watoto wetu ambao ndio wananchi wetu,"amesema.


Awali, akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Mhandisi  Stephano Kaliwa amesema wamepokea sh.milioni 475.3 kwa maelekezo ya kujenga shule mpya ya msingi yenye vyumba vya madarasa 16, vyumba 2 vya madarasa ya awali, jengo la utawala, matundu ya vyoo 28.


Amesema, mradi huo kukamilika kwake umekua na faida ya kuondokana na  msongamano wa wanafunzi darasani,  kusogeza huduma ya shule karibu katika jamii na kuongeza kiwango cha uandikishaji wa watoto wenye umri wa kwenda shule.


Post a Comment

0 Comments