MAKAMU MWENYEKITI WA SIMBA YA FAINALI CAF 1993 AFARIKI DUNIA

 


Na mwandishi wetu

ALIYEWAHI kuwa Makamu Mwenyekiti wa Simba SC miaka ya 1990, Fakhruddin Amijee amefariki dunia jana jioni nyumbani kwake Arusha akiwa ana umri wa miaka 84 baada ya kuusmbuliwa na maradhi kwa muda mdupi .
Amijee aliyewahi pia kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wavu Dar es Salaam (TAREVA) na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Kikapu Tanzania (TABA) amezikwa jana hiyo hiyo usiku Jijini Arusha.
Amijee alikuwa Makamu Mwenyekiti Simba kuanzia mwaka 1990 chini Mikidadi Kasanda, Juma Salum baadaye chini ya Ally Amir ‘Bamchawi’ na Priva Mtema (wote marehemu) mwaka 1996 na baada ya hapo akahamia kwenye michezo mingine na kuongoza TAVA na TABA.Post a Comment

0 Comments