RAIS DK.MWINYI APONGEZWA KWA KAZI NZURI NA VETERAN ZANZIBAR.

 


*RAIS DK.MWINYI APONGEZWA KWA KAZI NZURI NA VETERAN ZANZIBAR*. 


Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema amefarijika kwa Jumuiya ya Veteran Young Pioneers Zanzibar kumpongeza kwa kutekeleza vizuri ilani ya uchaguzi ya Ccm katika kipindi cha miaka mitatu kwa miradi mbalimbali ya maendeleo. 


Rais Dk.Mwinyi amesema hayo  alipokutana na Maveterani hao wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Khamis Rajab Mnubi Ikulu Zanzibar tarehe: 28 Februari 2024.


Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema ataongeza kasi ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo  kwa kutekeleza ahadi zote alizowaahidi wananchi wa Zanzibar. 


Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi ameipongeza Jumuiya hiyo kwa kuendeleza majukumu ya kujitolea kuwafundisha vijana uzalendo, ukakamavu  na itikadi ya Chama.  


Jumuiya ya Veteran Young Pioneers ilianzishwa rasmi tarehe 20 Desemba mwaka 2015 chini ya sheria No:6 ya 1995 kwa kujumuisha wanachama ambao wametokana na Umoja wa Young Pioneers ulioasisiwa tarehe 01 Machi 1964 mara baada ya Mapinduzi Matukufu kwa lengo la malezi ya vijana katika maadili mema, uzalendo na itikadi ya Chama.
🗓️28 Februari 2024


📍Ikulu, Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments