SIJARIDHISHWA NA MAKISIO YA GHARAMA ZA UJENZI- Dk Mfaume

 
 Na Angela Msimbira, ARUSHA


Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais -TAMISEMI  Dkt. Rashid Mfaume hajaridhishwa na tabia ya baadhi ya Waandisi wa  Halmashauri ya Jiji la Arusha  kuandaliwa na kufanyiwa makisio ya gharama za michoro ya huduma na mkandarasi. 

Hali hiyo imefanya makadirio ya gharama za ujenzi kuwa kubwa na kuitia hasara Serikari. 


Dkt. Mfaume ameyasema hayo leo Februari 26,2024  alipokuwa akikagua miradi ya ujenzi na huduma zinazotolewa  kwenye vituo vya kutolea huduma za afya mkoani Arusha


Amesema makadirio hayo huwa yanafanywa na Mhandisi wa Halmashauri na mkandarasi hapaswi kundaa makadrio hayo baada ya kukabithiwa kazi kwa kuwa inaongeza gharama za mradi. 


Akikagua ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje kwenye Kituo cha Afya Levolosi amesema: " inasikitisha kazi ambayo inatakiwa kufanywa na mhandisi inafanywa na mkandarasi, hili halikubaliki ni kosa kisheria." 


Kuhusu ujenzi wa jengo hilo, Dkt. Mfaume amesikitishwa na kasi ndogo ya ujenzi wa jengo hilo ambalo lilitengewa fedha mwaka 2022/2023 lakini mpaka leo jengo hilo lipo katika hatua ya msingi. 


Pia Mkurugenzi hajafurahishwa na Halmashauri kutokuwa na vikao rasmu na Mkandarasi vya kufuatilia utekelezaji wa mradi kutoka mradi huo uanze, jambo ambalo limechangia mradi kuchukua muda mrefu kukamilika.


Aidha, Dkt. Mfaume amezitaka Timu za usimamizi na uratibu wa shughuli za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii ngazi ya Halmashauri (CHMT) na Mkoa (RHMT) kufanya ufuatiliaji na usimamizi wa mara kwa mara ili kuhakikisha.


Kituo cha afya Levolosi kimepokea  shilingi milioni 642 kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la  wagonjwa wa nje kati ya fedha hizo  kiasi cha shilingi milioni 500 ni fedha toka Serikali kuu na shilingi milioni 142 ni fedha za mapato ya ndani.

Post a Comment

0 Comments