TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMANNE FEBRUARY 27,2024

 


Real Madrid wamefikia makubaliano ya kumsajili beki wa Bayern Munich na Canada Alphonso Davies, 23, na watatarajia kukamilisha dili hilo msimu huu wa joto au 2025, atakapokuwa mchezaji huru. (Athletic- Usajili unahitajika)

Mustakabali wa kocha wa Chelsea Mauricio Pochettino haujulikani baada ya timu yake kupoteza mchezo wa fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Liverpool, huku kocha wa Sporting Lisbon Ruben Amorim akitarajiwa kuchukua nafasi yake. (Mail)

Manchester United inatarajiwa kuwatoa wachezaji kadhaa msimu huu huku winga wa Brazil Antony, 24, akiwa miongoni mwa wale ambao watakuwa tayari kuwauza. (MEN)

Chelsea wanatumai kumuuza mlinzi Trevoh Chalobah, 24, na mshambuliaji wa Albania Armando Broja, huku mustakabali wa kiungo wa Uingereza Conor Gallagher, 24, na beki wa Uhispania Marc Cucurella, 25, ukiwa mashakani wanatarajia kufanya mabadiliko makubwa msimu huu wa joto. (Telegraph - usajili unahitajika)


Bayern Munich, Liverpool na Arsenal wako kwenye mbio za kumnunua kiungo wa kati wa Fulham na Ureno Joao Palhinha, 28, msimu huu wa joto. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Manchester City Kevin de Bruyne angependelea kuhamia Major League Soccer (MLS) badala ya Ligi Kuu ya Saudi Pro. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji anatimiza miaka 33 msimu huu wa joto, wakati mkataba wake unaingia mwaka wake wa mwisho. ( Athletic- Usajili unahitajika)Post a Comment

0 Comments