TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATANO 14,2024

 


Tottenham watamnunua Conor Gallagher wa Chelsea msimu huu wa joto ikiwa kiungo huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 24 hataafikiana na The Blues kuhusu kuongeza mkataba wake wa sasa, ambao unamalizika mwishoni mwa msimu ujao. (Telegraph - usajili unahitajika)

Manchester City wamekubali mkataba wa kumnunua winga wa Brazil Savio, 19, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo katika klabu ya Girona ya Uhispania kutoka Troyes ya Ufaransa. (Fabrizio Romano)

Newcastle wameungana na West Ham katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Genoa wa Iceland Albert Gudmundsson, 26. (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)

Arsenal wanafikiria kumuuza kiungo wa kati wa Ujerumani Kai Havertz mwenye umri wa miaka 24 msimu huu wa joto. (Fichajes - kwa Kihispania)

Wawakilishi wa Kylian Mbappe waliwasiliana na Liverpool kuhusu uhamisho mwaka jana, lakini klabu hiyo haikutaka kuvuruga mkakati wao mzima wa kifedha ili kumsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 wa Paris St-Germain na Ufaransa. (Independent)

Barcelona hawana uwezo wa kumteua Roberto de Zerbi kama kocha wao mpya kwa sababu ya kitita kinacohitajika ili kumpata kocha wa Brighton. (Matteo Moretto)

Crystal Palace wamechanganyikiwa katika jitihada zao za kumshawishi Kieran McKenna kuondoka Ipswich na kuchukua nafasi ya Roy Hodgson kama kocha lakini wanatumai raia huyo wa Ireland Kaskazini anaweza kuchukua mikoba mwishoni mwa msimu huu. (Guardian

Newcastle na Arsenal wako macho baada ya mazungumzo ya kandarasi kati ya Brentford na mshambuliaji wao wa Uingereza Ivan Toney, 27, kukwama. (TeamTalk)

Brentford imemtambua mshambuliaji wa Lille wa Canada Jonathan David, 24, kama mbadala wake iwapo Toney ataondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto. (Football Transfers)Post a Comment

0 Comments