TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATATU FEBRUARY 12,2024

 


Mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, 25, bado hajakubali masharti ya kujiunga na Real Madrid mkataba wake utakapomalizika huku klabu hiyo ya La Liga ikihangaika kufanya mazungumzo na mamake mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, na wakala, Fayza Lamari. (Marca)

Mkufunzi wa Real Madrid Carlo Ancelotti amedokeza kuwa timu hiyo haimhitaji Mbappe kwani tayari wana "wachezaji sita bora duniani". (Goal)

Kinda wa AC Milan Francesco Camarda atatia saini mkataba wake wa kwanza wa kitaalamu na Rossoneri wakati chipukizi huyo wa Kiitaliano atakapofikisha umri wa miaka 16 mwezi ujao licha ya Manchester City na Borussia Dortmund kumtaka. (Calciomercato, via Football Italia)

Arsenal na Chelsea ni miongoni mwa vilabu vinavyomnyatia winga wa Athletic Bilbao Nico Williams, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 akionekana kuwa bora kwa Ligi ya Premia. (Fabrizio Romano, via CaughtOffside)


Post a Comment

0 Comments