BODI YA SUKARI YAENDESHA OPERESHENI KWA WAFANYABIASHARA WANAOKIUKA BEI ELEKEZI YA SUKARI

 Na mwandishi wetu,Dar es salaam

Bodi ya Sukari imeendelea na msako mkali Nchini dhidi ya baadhi ya wafanyabiashara wanaouza bidhaa ya Sukari nnje ya Bei elekezi.Msako huo umefanyika leo Jumatano February 14,2024 Katika maeneo ya Mbagala na Tandika Sokoni wilayani Temeke Jijini Dar es salaam.


Bei Elekezi ya Sukari kwa kilo Moja ni shillingi  za kitanzania 3000,Hivyo Kuna baadhi ya wafanyabiashara wanauza  Sukari kilo Moja Tsh 4,000 na pia Serikali imebainika Kuna udanganyifu mkubwa wafanyabiashara wa Sukari ikiwa pamoja na uchakachuaji wa mashine za kielektroniki kwa kutoa risiti zisizo halisi kulingana na mzigo husika.Takribani watu saba wamekamatwa katika msako mkali ambapo Mbagala wamekamatwa watatu na Tandika wamekamatwa wanne Jumla waliotiwa nguvuni katika msako huo ni watu saba.Akizungumza Afisa wa bodi ya Sukari Eng.James Mwera amesema "Sisi tunachokifanya ni kuweza kuwakamata wale wafanyabiashara wanokiuka Bei elekezi iliyotolewa na BODI ya Sukari,kama tunavyofahamu Bei ya Sukari kwa kilo Moja inauzwa kuanzia  tsh 2,700 mpaka 3,000 hii ndio Bei elekezi ya bodi ya sukari  na kwa Bei ya Jumla kwa Mfuko WA kilo 25 inauzwa 70,000 na Mfuko WA kilo 50 ni  Tsh 140,000 isizidi hapo na ukiuza zaidi ya hapo utakuwa unakiuka Bei elekezi hivyo ndugu Wananchi ukiuzia zaidi ya Bei hiyo usinunue ikiwezekana uripoti Bodi ya sukari au kituo Cha Polisi kilicho karibu yako"


"Mpaka sasa hivi Tumekamata wafanyabiashara saba ambapo operesheni tumeiendesha Tandika na Mbagala kwa hiyo wafanyabiashara Wana kesi ya Kujibu kwa sababu wanauza Bei isiyo elekezi iliyopangwa na Serikali,sababu za  Wafanyabiashara kukiuka Bei elekezi niweze kusema baadhi yao inakuwa nia sab ya Tamaa ya kupata pesa zaidi  "alisema James Mwera   

 


Aidha kwa upande mwingine Afisa kutoka Bodi ya Sukari Tumwendeli Gilla ametoa Rai kwa wafanyabiashara wengine wafate maagizo ambayo Serikali imeyatoa ya Bei elekezi ya Sukari isiyozidi tsh 3,000 kwa rejareja na kwa Bei ya Jumla isizidi 2,800.

Naye mkazi wa Tandika Dotto Kimbanga ameipongeza Bodi ya sukari kwa Hatua wanazochukua kwa wafanyabiashara wanaoikiuka Bei elekezi kwani upandishaji WA Bei kiholela inamkandamizi na kumbebesha mzigo kwa Wananchi.


Post a Comment

0 Comments