WAFANYABIASHARA MSIPANDISHE BEI ZA VYAKULA

 Na mwandishi wetu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itashughulikia changamoto zote za wafanyabiashara wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa bandari ya Malindi  ikiwemo kufanya kazi usiku kwa kuwekewa taa na  kazi kuendelea siku ya jumapili.


Rais Dk.Mwinyi amesema hayo akizungumza na  Jumuiya ya ushirika wa Majahazi na Wafanyabiashara katika bandari ya Malindi pia amezungumza na Wafanyabiashara wa soko kuu la Darajani katika mwendelezo wa ziara yake maalumu  ya kutembelea masoko na  kusikiliza changamoto zao Mkoa wa Mjini tarehe: 26 Februari 2024.


Aidha Rais Dk.Mwinyi amewaomba wafanyabiashara kutopandisha bei ya vyakula katika kuwahurumia na kuwasaidia wananchi wanyonge kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhan .


Rais Dk.Mwinyi ametoa maagizo kwa Taasisi ya uwezeshaji wananchi kiuchumi (ZEEA) kuwapatia mikopo wafanyabiashara walio kwenye maeneo maalumu ya biashara. 


Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amewataka viongozi  wa Manispaa, Wilaya, Mkoa kuwapanga Wafanyabiashara kwa kuwawekea mazingira mazuri ya kufanya biashara zao.

🗓️26 Februari 2024


📍Mkoa wa Mjini Magharibi.

Post a Comment

0 Comments