WAGANGA WAFAWIDHI KUANZA KULIPWA POSHO YA MADARAKA

 


Na mwandishi wetu


Serikali kupitia Wizara ya Afya imesema kuanzia mwaka wa fedha ujao waganga wafawidhi katika vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi wataanza kupewa posho ya madaraka kwa kazi kubwa wanayofanya kwenye ngazi ya msingi.


Akizungumza katika Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wafawidhi wa Vituo vya kutolea huduma za Afya ngazi ya msingi mapema leo hii Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema waganga wafawidhi wanastahili kulipwa posho hiyo na ameahidi kuanzia July,2024 itaanza kutolewa kwa wataalam hao muhimu.


‘Amesema Wanganga Wafawidhi mnafanya kazi kubwa kwenye vituo vya kutolea huduma ninyi ndio madaktari, wafamasia, wataalam wa maabara, mnasimamia ujenzi wa miradi ya serikali hakika mnastahili kulipwa posho hii naenda kuonana na wadau na katika fedha tutakazopata kiasi kitatumika kwa ajili ya kulipa posho hii’ amesisitiza Mhe. Ummy


Na kwa kuwa sasa ndio tunaendelea na michakato ya Bajeti posho hii iingizwe kwenye mipango yetu imi iwe rasmi na watalaam wetu hawa wapate posho hii’ alisisitiza Mhe. Ummy
Post a Comment

0 Comments