ARSENAL FIKRA ZA KUMNUNUA MLINZI WA KATI WA SPORTING LISBON MWAIVORY COAST DIOMANDE

 


The Gunners wanafikiria kumnunua mlinzi wa kati wa Sporting Lisbon na Ivory Coast Ousmane Diomande, 20, baada ya kushuhudia makali yake katika safari ya kumtazama mshambuliaji wa Uswidi Viktor Gyokeres, 25. (Sun).

Gyokeres amempita mshambuliaji wa England na Brentford, Ivan Toney kwenye orodha ya washambuliaji wapya wanaotarajiwa kuwa wa Arsenal , huku West Ham pia wakimtaka. (TalkSport)

Manchester United italeta kikosi kizima cha kiufundi cha England ikiwa watamteua Gareth Southgate kama meneja katika msimu wa joto.(Sun)

Lakini United wanataka kuzungumza na meneja wa Wolves Gary O'Neil kuhusu jukumu katika safu mpya ya ukufunzi huko Old Trafford. (ESPN)

Meneja wa zamani wa Chelsea, Manchester United na Tottenham Jose Mourinho anasema yuko tayari kurejea kufundisha msimu huu wa joto kufuatia kuondoka kwake kutoka Roma. (Fabrizio Romano)

Pamoja na wote wanaomtaka meneja wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso, Liverpool na Bayern Munich wanamtaka kocha wa Brighton Roberto de Zerbi kama mbadala wake. (Bild - kwa Kijerumani)

Post a Comment

0 Comments