BENKI YA KCB YAJA NA MIKAKATI BORA KWA WATEJA WAKE,YAZIDI KUCHANJA MBUGA KWENYE HUDUMA.

 


Na mwandishi wetu

Katika kuhakikisha wanawapa faraja wateja wake,Benki ya KCB inaendelea kuwa wabunifu kwa kuleta Suluhu mbalimbali za kuwafaa wateja wake nchini pamoja na kuboresha mitandao yake ili mteja aweze kuendesha biashara kwa ufanisi zaidi.


Hayo yamebainishwa na  Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Bank, Abdul Juma ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo na wa kati KCB Bank wakati wa futari waliyoiandaa Benki hiyo kwa wateja wake hapo Juzi Jijini Dar es Salaam.


"Tunatambua kuwa taknolojia ni kitu muhimu sana kwa mteja wetu ili aweze kuendesha biashara kwa ufanisi zaidi hivyo sisi KCB bank tunaendelea kuwa wabunifu kwa kuleta Suluhu mbalimbali za kuwafaa wateja wetu nchini pamoja na kuboresha mitandao yetu kwa kuwa Dunia sasa imekuwa kiganjani, wateja wanahitaji kupata huduma za kibenki palepale walipo hivyo kcb inawaletea huduma kama internet banking, mobile banking, kcb visa card, na KCB wakala ili tuweze kuwafikia wateja wetu kule walipo na wao wafanye biashara na KCB  wakiwa ukouko walipo" Alisema Abdul 


Aidha,Abdul amesema Benki hiyo imeendelea kuwa mstari wa mbele katika ubunifu na kubuni huduma mbalimbali ambazo zinachochea maendeleo ya wateja na nchi kwa ujumla, ambapo mbali na huduma za kawaida wanazozitoa, Benki yao imekuwa mstari wa mbele kwa kuleta huduma za kibunifu ili kuongeza tija katika soko ikiwemo huduma zinazozingatia sharia kupitia kitengo chao cha Sahal banking.


"Mfano wa huduma za kimageuzi, bidhaa ya fursa sukuk mwaka 2022 banki yetu ilizindua hati fungani ya kwanza ya kiislam Tanzania ambayo ililenga kukusanya kiasi Cha shilingi milioni 10 kwaajili ya kuongeza uwekezaji kwa Idara yetu ya sahal banking"


"Tumefikia malengo na tumezidi kwa asilimia 10 na hati fungani yetu hii imeorodheshwa kwenye soko la hisa DSE hii inaonyesha Imani kubwa ambayo watanzania wametuamini"


Hata hivyo,Abdul amesema Benki yao imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuleta huduma na bidhaa za kibenki ambazo zinawasaidia wateja kufanikisha malengo ya kibiashara au malengo binafsi kwa urahisi zaidi, ikiwemo huduma za ufadhili, zilizoletwa mahususi kumrahisishia mfanyabiashara kurahisisha malengo kwa kufata misingi ya Imani ya kiislam.


Huku naye Mkuu wa Kitengo cha KCB Sahl Banking Amour Muro

 amewaomba wateja wote kunufaika na fursa  kubwa ya kubenki na KCB Sahal banking ili kuendana na misingi mizuri ya kiisalm.


"Idara ya KCB Sahal Banking, tunatoa huduma za kifedha au kulipa riba kwa wateja mbalimbali ikiwemo watu binafsi, wafanyabiashara, makampuni madogo na makubwa, vikundi maalumu, wazazi, wanafunzi, wafanyakazi n.k, huduma zetu zimegawanyika sehemu 3, huduma za kimiamala za Bank, huduma za akiba na uwekezaji, na huduma za mikopo zisizotoza riba kupitia misingi ya kiislam"


Pamoja Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Shariah ya KCB Sahl Banking Sheikh Khamis Mataka aliwataka wateja wote washirikiane na Benki ya KCB katika kupata huduma ambazo ni Bora na ambazo zinakidhi matakwa ya kisheria.


"Kwa niaba ya Bodi ya sharia kcb, nawahakikishia huduma na Miamala inayotendwa na KCB ni miamala yenye kuzingatia sharia ya kiislam, 


KCB wapo sambamba na sharia na wanaendelea katika hali kama hiyo, tunaipongeza sana Menejimenti namna ambavyo inachukua hatua mbalimbali kuhakikisha kwamba miamala inayofanywa inazingatia sharia"


Mwenyekiti wa Bodi Benki ya wakurugenzi kutoka Benki ya KCB, John Ulanga alisema wao kama Benki ya KCB wataendelea na utamaduni wa kukua mwaka hadi mwaka na kuja nabidhaa mpya ndani ya sahal Banking.

Post a Comment

0 Comments