DANCE CLUB YAZINDUA KAMPENI MAALUM "DANCE CLUB TUVUSHE" KUELEKEA ROBO FAINAL YA KLABU BINGWA

 Na mwandishi wetu

Baa Maarufu jijini Dar es salaam ya Dance Club imekuja na kampeni Maalumu ya kuhamasisha mashabiki wa timu za simba na yanga katika Michezo yao ya robo fainali ili kufuzu hatua ya nusu fainali.


Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam meneja wa matukio na burudani wa Bar hiyo Jafar amesema lengo la kuja na kampeni hiyo iliyopewa jina la  'Dance club Tuvushe' ni ili kutoa chachu kwa mashabiki wa vilabu vya Simba na Yanga kuhakikisha wanahamasika kusapoti timu zao.


Amesema kuwa katika kampeni hiyo wametoa kadi maalum kwa mashabiki wa timu hizo ambazo zitawawezesha kuangalia michezo ya hatua ya robo fainali ya katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika kupitia screen kubwa zitakazofungwa ndani ya Bar hiyo.


"Tumeanzisha kampeni hii ili kuhakikisha mashabiki wanahamasika tutatoa kadi ambazo zitauzwa kwa shilingi elfu kumi na tutatoa fursa kwao mashabiki kuja kuhakikisha timu zao zinafuzu kwenda hatua ya nusu fainali na yote watayaona hapa hapa dance club"alisema meneja huyo.


Kwa upande wao mashabiki wa timu za Simba na Yanga wamepongeza hatua ya bar hiyo kuja na kampeni hiyo huku wakiwataka mashabiki wenzao kujitokeza kwa wingi kuangalia mechi baina ya timu zao na mahasimu wao.


"Sisi kama Simba SC tutahakikisha timu yetu inamkalisha Al Ahly kwa Mkapa kwani pale hatokagi mtu na tuna historia ya kumfunga Ahly naamini tutafuzu kwenda nusu fainali"alisema Albert Oscar ambaye ni shabiki wa Simba.


Naye Shabiki wa Yanga Shaban amesema Mamelodi hawatatoka salama ndani ya dimba la Mkapa March 30 kwani watahakikisha wanawapiga nje ndani.

Post a Comment

0 Comments