DC KATWALE ASISITIZA VYOMBO VYA USALAMA KUTENDA HAKI .

  Na Joel Maduka ,TABORA.


Mkuu wa wilaya ya Tabora Deusdedith Katwale  amevitaka vyombo vya usalama kuendelea kutenda haki na  kusimamia misingi  imara ya kazi zao likiwemo suala la nidhamu.


Mhe,Katwale ametoa Rai hiyo wakati alipokutana na viongozi wa Jeshi la Polisi Wilayani humo pamoja na viombo vingine vya ulinzi na usalala ,amesema wajibu wao kama askari ni kuhakikisha wanalinda amani ya wananchi pamoja na kushughulika na vitendo vyote vya uharifu.


"Kwa kutambua ubora na ujuzi wenu kama askari  ndio maana nikasema siwezi kufanya kazi hii pekee nikajuwa nawahitaji ninyi ili kufanikisha suala zima la ulinzi na usalama kwenye Wilaya yetu”Deusdedith Katwale Mkuu wa Wilaya ya Tabora.


 


Aidha Katwale ameongeza kwa kuwashukuru  Kwa kazi nzito ambayo wameendelea kuifanya ya kulinda raia na Mali  kutokana na kazi hiyo mara kadhaa wameendelea kupitia nyakati ngumu  pamoja na mazingira magumu ya kazi zao.


“Niwaombe OCD Mussa Kyando na Kikosi chako kizima na watumishi wengine mhakikishe mnaitumikia nchi  Kwa uadilifu  na uzalendo, Hapa  ningependa kusema jambo nikiwa katika Wilaya hii ningependa kuona tukishirikiana kuhakikisha tunapambana kudhibiti suala la wahamiaji haramu nikiwa katika wilaya hii sitapenda kuona mnafumbia Macho suala la watu ambao wamekuwa wakiingia nchini bila ya vibali” Deusdedith Katwale Mkuu wa Wilaya ya Tabora.


 


Kwa upande wake  OCD wa wilaya ya Tabora Mussa Kyando ametumia nafasi hiyo kumshukuru Mkuu wa Wilaya kwa namna alivyowiwa  kukutana nao na kusikiliza kero ambazo zinawasibu kwenye shughuli zao huku akimhakikishia kumpa ushirikiano katika suala la ulinzi na usalama.“Mimi na askari wenzangu pia watumishi wengine wote tunakuahidi ushiahirikiano mkubwa na Kwa maagizo uliyotoa na ushauri pia tumepokea  sisi tunachoweza sema ni kazi tutaifanya Kwa Uadilifu na Uzalendo”Mussa Kyando OCD Wilaya ya Tabora.

 Post a Comment

0 Comments