DIMWA AMEWATAKA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU KUKITHIRISHA KUFANYA IBADA

 
Na mwandishi wetu

Naibu Katibu Mkuu wa chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Mohammed said Dimwa amewataka Waumini wa Dini ya Kiislamu nchini kukithirisha kufanya ibada hasa katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili kuweza kupata fadhila za Mwenyezi Mungu.


Akitoa nasaha kwa Viongozi, na Wanachama mara baada ya Dua ya kuwaombea Viongozi wa Nchi na Iftar iliyondaliwa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Taifa (UVCCM) huko Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul-wakil Kikwajuni amewataka kufanya ibada ili kufikia Ucha Mungu.


Aidha amesema Ramadhani inakaribia kumalizika na hakuna mtu yoyote mwenye uhakika wa kufika Ramadhani nyengine hivyo ni vyema kuendeleza kufanya mambo mema anayoyaridhia Mwenyezi Mungu ikiwemo kusimamisha Swala tano, kutoa zaka na sadaka, kusoma Qur-an kwa wingi na kuenda Makka kuhiji kwa Mwenye uwezo hata baada ya kumalizika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.


Sambamba na hayo amewasihi Wazee kuwa na malezi mema kwa watoto wao pamoja na kuwataka Vijana Kuwatii Wazee na kufuata maamrisho ya Qur-an ili kupata radhi za Allah.


Hata hivyo Naibu Katibu Mkuu huyo amewasihi Wanachama wa CCM kuendelea kuwa pamoja na kushikamana kuanzia Chama na Jumuiya zake ili kuzidi kushika Dola na kuwa karibu na kuwajali Wazee waliostahafu  kukitumikia chama hicho ili kupata fikra na mbinu mbalimbali waliotumia wa Uongozi wao.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa umoja wa Vijana Taifa Mohammed Ali Kawaida amewaomba wenye uwezo kuendeleza kuftarisha katika siku zilizobakia za mwezi mtukufu wa Ramadhan kwani kitendo hicho ni miongoni mwa ibada inayojenga   upendo, umoja na Mshikamano.


Aidha amewaomba Waumini wa dini ya kiislam kuutumia mwezi huo kuwaombea viongozi wa Nchi dua ili Allah SW awawezeshe kuendelea kuiongoza nchi katika misingi mema.


"Viongozi wetu wakuu wanakazi ngumu Sana ya kuiongoza Nchi Wajibu wetu Sisi kuwasaidia kwa kuwaombea dua ili Mwenyezi Mungu awape utulivu na uwezo wa kutekeleza majuku yao mazito." Alisema Kawaida


Nao Baadhi ya Washiriki katika iftari hiyo wameshukuru na kuupongeza Uongozi wa UVCCM Taifa kwa kuandaa iftari hiyo kwani imeweza kuwakutanisha pamoja na kujenga Upendo na faraja baina yao.@uvccm_zanzibar 

@ccm_zanzibar

Post a Comment

0 Comments