DKT MAHERA AAGIZA USIMAMIZI DHABITI MIRADI YA AFYA

 


Angela Msimbira GEITA


Timu za Usimamizi wa Huduma ya Afya za Mikoa na Halmashauri zimetakiwa kusimamia miradi ya afya inaxyotekelezwa kwenye maeneo yao. 


Akizungumza na Timu ya Mkoa wa Geita, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia afya Dkt.Charles Mahera amesema Serikali imewekeza fedha katika kuboresha afyamsingi hivyo kila mtumishi anawajibu wa kuhakikisha miradi ya afya inakamilika kwa wakati na ubora. 


Pia amewaonya viongozi hao kujiepusha na rushwa ambazo zinaleta taswira mbaya kwa jamii kuwa bila kutoa fedha huwezi kupata Huduma kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali.


Dkt.Mahera amewataka kuhakikisha vituo vyote vya kutolea huduma za afya ambavyo vimekamilika na havitoi huduma kwa wananchi vianze kufanyakazi mara moja.


Pia amewataka kuhakikisha wanafanya msawazo wa watumishi ndani ya halmashauri ili vituo ambavyo havina watumishi wa kutosha viweze kupata watumishi na kuanza kutoa huduma  za msingi zinazohitajika kwa wananchi.

Post a Comment

0 Comments