RAIS DK. MWINYI APOKEA SALAMU ZA POLE KUTOKA KWA CDF

 Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na 
Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi @dr.hmwinyi amepokea salamu za pole nyumbani kwake Migombani kutoka kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali John Jacob Mkunda kufuatia kifo cha Baba Mzazi, Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassani Mwinyi aliyefariki dunia tarehe: 29 Februari 2024, Dar es Salaam na kuzikwa tarehe: 02 Machi 2024, Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini, Unguja.
 

📅 05 Machi 2024
📍Ikulu, Migombani

Post a Comment

0 Comments