FCS YATANGAZA KUPATA MKURUGENZI MPYA,KIWANGA AAGA HUKU AKIMTAJA RAIS SAMIA.

 


Na mwandishi wetu

SHIRIKA la Foundation for Civil Society (FCS),limetangaza kupata mkurugenzi mpya Justice Rutenge,huku aliyekuwa mkurugenzi wake, Francis Kiwanga,ameomba kustaafu ndani ya shirika hilo.Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam ,Mwenyekiti wa bodi ya FCS, DKt. Ally Laay,amesema Kiwanga ameomba kustaafu baada kulitumikia shirika hilo kwa mafanikio makubwa  ndani ya miaka tisa.


Aidha,Dkt Laay,amesema Bodi hiyo baada kupata maombi ya Kiwanga ikaitangaza nafasi hiyo na kuruhusu watu wenye sifa waweze kuomba.


"Watu waliomba walikuwa hamsini tukachuja mpaka wakabaki sita ndio tukafanikiwa kupata huyu Mtendaji mpya wa FCS Justice Rutenge,"Amesema 


Akimzungumzia Mkurugenzi huyo mpya,Dkt Laay,amesema bodi imemwamini kuwa atafanya kazi vizuri na kuendelea aliposhia Kiwanga kutokana na sifa alizo nazo na ni kijana na anatarajia kuanza kazi mwezi wa tano” amesema Laay.


Kwa Upande Mkurugenzi Mtendaji wa FCS anayemaliza muda wake wa uongozi Francis Kiwanga,ameishukuru bodi hiyo na watendaji FCS na asasi zote za kiraia kwa kumpa ushirikiano kwa kipindi chote cha miaka 9 alichodumu nacho.


Pia Kiwanga, amesema Shirika la Asasi za Kiraia nchini (FCS) linajivunia miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuheshimu na kusimamia misingi ya demokrasia.


Amesema kuwa FCS inajivunia uongozi wa Rais Samia unaoheshimu misingi ya democrasia na uhuru wa watu, ambapo amebainisha kuwa FCS itaendelea kuwa daraja kati ya watu na serikali katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.


Naye Mkurugenzi Mtendaji mpya wa FCS Justice Rutenge, ameahidi kufanya kazi kwa weledi kulingana na taaluma na ujuzi alio nao kwa maslahi mapana ya jamii na serikali kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments