HAALAND KUTHIBITISHA UWEZO WAKE KWA REAL MADRID

 


Mshambulizi wa Norway Erling Haaland, 23, anatazama robo fainali ya Ligi ya Mabingwa ya Manchester City akiwa na Real Madrid kama fursa ya kuthibitisha uwezo wake wa kuhamia miamba hao wa Uhispania. (AS - kwa Kihispania)

West Ham wanatarajia winga wa Algeria mwenye umri wa miaka 28 Said Benrahma kusaini mkataba wa kudumu katika klabu ya Ligue 1 ya Lyon msimu huu wa joto.(Football Insider)

Bayer Leverkusen ni miongoni mwa vilabu vya juu vya Ulaya vinavyotaka kumsajili mlinda lango wa Everton wa England wa kikosi cha chini ya umri wa miaka 17 Douglas Lukjanciks, 16, msimu huu(Mail)

Meneja wa Brighton Roberto de Zerbi "amefurahishwa" na nia ya Bayern Munich kutaka huduma zake - lakini kocha huyo wa Italia hana haraka ya kufanya uamuzi juu ya mustakabali wake wa muda mrefu.(Mirror)

Post a Comment

0 Comments