JAMII YA WAFUGAJI WAISHUKURU SERIKALI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA BOOST.

 Na mwandishi wetu

Jamii ya wafugaji katika Kijiji cha Kihumbu wilayani Bunda mkoani Mara wameishukuru Serikali kwa kuwajengea shule kupitia mradi wa BOOST ambayo imewaondolea watoto kutembea  umbali wa kilomita10  kufuata elimu.

Kauli hiyo imetolewa na wakazi wa Kijiji cha Kihumbu ambao wamesema awali watoto wao walilazimika kutembea umbali kilomita 10 kwenda shule mama hali iliyopelekea wengi wao  kukatisha masomo hususani jamii hiyo ya wafugaji.

"Tulijitolea eneo la kujenga shule baada ya kuanzisha darasa la utayari kutokana na umbali watoto wetu walikuwa wanaumia sana. na Sisi tuko pembezo mwa Hifadhi ya Serengeti na kuna wakati watoto walikuwa wanakutana na tembo," amesema Kiteta Thomas. 

Awali akitoa Taarifa kwa timu ya ufatiliaji kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia na Benki ya Dunia, Mkuu wa Shule ya Msingi Saba Sita, Gatrida Maregesi amesema ujenzi wa shule hiyo umeongeza maudhurio ya wanafunzi kuanzia darasa la awali hadi la Saba na kupunguza utoro shuleni hapo.

Naye mtalam elimu kutoka Benki  ya Dunia, Gemma Todd ameipongeza serikali kwa usimamizi uliotukuka wa utekelezaji wa mradi  wa BOOST huku akiomba serikali kuangalia namna ya kuhakikisha shule hiyo inakapata maji ili kuwahudumia wanafunzi ikiwa niutekelezaji wa afua zinazohitajika.

Aidha akizungumza na wananchi katika eneo la Shule ya Msingi  Saba Sita, Mkurugenzi Msaidizi anayesimamaia Elimu ya Awali na Msingi  Bi.Susana Nussu amewataka wazazi wote l kukemea vitendo vya utoro kwa watoto wao kwa kuwa serikali imewekeza fedha nyingi kuhakikisha watoto wao wanapata elimu bora.


Post a Comment

0 Comments