KAMPUNI YA TVS NA CAR & GENERAL WAZINDUA MAFUTA YA INJINI TRU4 OIL 20W 50

 
TVS YAZINDUA MAFUTA YA INJINI TRU4 OIL 20W 50


Kampuni ya Car & General Trading Ltd na TVS MOTOR Company ltd yazindua mafuta ya injini kwa soko la Tanzania,Halfa hiyo imefanyika Leo Jumatano March 27,2024 Katika mgahawa wa Akemi  Golden Jubilee Posta Jijini Dar es salaam.

Kampuni ya Car & General imekuwa mstari wa  mbele Katika Kutoa huduma ya uzalishaji wa umeme wa magari na uhandisi Katika ukanda huu wa Afrika mashariki na pia ni wasambazaji pekee wa bidhaa za kampuni ya TVS ambazo ni pikipiki za miguu miwili na mitatu pamoja na vipuri kwa Tanzania Bara na visiwani Zanzibar.


Kampuni ya TVS ni kampuni kutoka India ambayo ina  nguzo ya uamunifu na uvumbuzi Katika Mazingira ya viwanda vya magurudumu mawili na Matatu pamoja na vifaa vya utengenezaji wa Hali ya juu kutoka India na Indonesia,Kampuni ya Tvs imeweza kuchonga urithi wa Karne na Karne uliyojizolea umaarufu Katika Maadili ya uaminifu ,thamani na huduma pia TVS inajulikana kwa kujitolea kwake Kutoa uzoefu Bora wa wateja Katika nchi zaidi ya 80 hivyo Tvs imeendelea kuweka alama za bidhaa zake za kimataifa.


Alama ya TVS ya bidhaa ya pikipiki ya magurudumu mawili na Matatu iko Katika injini zao ambayo inatoa nguvu isiyo kifani,mileage ya kipekee na thamani ya ajabu kwa Kutambua Umuhimu wa jukumu la lubrication ya injini Katika kuboresha utendaji na maisha marefu ya pikipiki kampuni ya  Car & general  kwa kushirikiana na TVS wamezindua TVS TRU 4 Oil 20W 50 ambayo imetengenezwa Mahususi kwa ajili ya injini ya TVS ya pikipiki ya magurudumu mawili na Matatu na imetengenezwa Nchini Tanzania na Total Energies mafuta yametengenezwa kukidhi viwango vya usahihi vya pikipiki ya TVS.


TVS TRU 4 Oil 20W 50 imeundwa ili kustawi chini ya joto la juu,kuhakikisha utendaji Bora Katika Hali ya kudai na uundaji wake ni wa Hali ya juu ambayo hupunguza msuguano,mchubuko na uchakavu wa vifaa vya injini wakati wa kuwezesha vilainishi kujiboresha na kupooza na Inapanua muda wa kubadilisha mafuta Hadi KM 5000 kwa mwenzi.

TVS TRU 4 Oil 20 W 50  inawapa wateja faida zinazoonekana ikiwa ni pamoja na Utendaji wa injini ulioimarishwa,Kupunguza mchubuko na uchakavu wa vifaa,upinzani wa joto la juu na ufanisi wa mafuta Bora kwa kukimbatia ubunifu huu Kuna tafsiri ya akiba kubwa ya gharama kwa wateja na uwezo wa kuokoa Hadi Tsh 10,000 kwa mwenzi.


Akizungumza na waandishi wa Habari Meneja wa Bajaji na Pikipiki kutoka TVS Bwana Jonathan Masanja amesema"TVS ni kampuni ya kibiashara ambayo ipo Tanzania tangu miaka ya 1960 na imekuwa na soko kubwa hapa Tanzania"


Post a Comment

0 Comments