KANISA LA AICT LAJITOSA KUSAIDIA WANAOISHI NA MAAMBUKIZI YA VVU.

 Na mwandishi wetu

Askofu wa kanisa la Afrika Inland Church (AICT) Dayosisi ya Geita,Reuben  Yusuf Ng’walla ,amesema jamii ya watu waishio visiwani katika ziwa Viktoria bado wanakabiliwa na changamoto ya magongwa ya mlipuko pamoja na janga la  ukimwi, jambo ambalo limesukuma kanisa hilo kukabiliana na magonjwa hayo.


Askofu Ng’walla ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuboresha maisha ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi (WAVIU) katika visiwa 10  ndani ya ziwa Viktoria upande wa Geita na Kagera.


Amesema kama kanisa bado wanakazi kubwa ya kuendelea kuwafikia watu wengi zaidi kwaajili ya kutoa elimu ya magonjwa ya mlipuko pamoja na janga la ukimwi.


“Tumeonelea kuzindua kampeni ya kuwasaidia watu ambao wameathirika na VVU sisi tunaamini maeneo ya visiwani ndio waathirika wakubwa wa magonjwa mbali mbali yanayoambukiza na yasiyoambukiza tunaimba serikali kuwekeza nguvu zaidi kusaidia maeneo ya visiwani kwani kuna watanzania wengi ambao wanaitaji elimu ya afya”Askofu Reuben Yusuf Ng’wallla.


Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela katika uzinduzi wa mradi, Mkuu wa Wilaya ya Chato Said Nkumba amesema kwa mujibu wa Takwimu za TACAIDS maambukizi ya VVU kwa Mkoa wa Geita yameshuka na kufikia asilimia 4.9.


Kwa upande wake mratibu wa afya visiwani ,Mch Samwel Limbe ameelezea madhumuni ya uwepo wa mradi huo wa kuwasaidia watu ambao wanamaambukizi ya VVU kwenye maeneo ya visiwani.


“Sisi tunaamini kuwa huduma hii ya kuwasaidia watu ambao wameathirika na maambukizi ya VVU itakuwa na tija na italeta mabadiliko kwenye maeneo ya visiwani kupitia meli yetu ya MV Jubilee ambayo imeendelea kutoa huduma za afya kwenye maeneo ya visiwa vilivyopo ziwa Viktoria”Mch Samweli Limbe Mratibu wa afya visiwani.


Kwa ushirikiano na serikali Kanisa la AICT Dayosisi ya Geita lmeendelea kutoa huduma za afya bure kwa wananchi wanaoishi visiwani, na sasa ni miaka tisa ya huduma kupitia meli ya MV  jublee hope.

Post a Comment

0 Comments