KHITMA YA DUA YA MAREHEMU MZEE ALI HASSAN MWINYI

KHITMA YA DUA YA MAREHEMU MZEE ALI HASSAN MWINYI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi amejumuika na waumini wa dini ya Kiislamu na waombolezaji katika Dua ya khitma ya kumuombea aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Mzee Ali Hassan Mwinyi ambayo inafanyika leo tarehe: 03 Machi 2024, katika viwanja vya maonesho Nyamanzi, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.

Dua hiyo imeandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kumuombea Marehemu Mzee Mwinyi ambaye amefariki dunia tarehe: 29 Februari 2024 katika hospitali ya Mzena, Dar es Salaam na kuzikwa tarehe: 02 Machi 2024 Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Aidha, dua hiyo umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama, Dini na wananchi. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisoma Juzuu wakati wa khitma ya Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Pili Hayati Ali Hassan Mwinyi aliyefariki tarehe 29 Februari 2024. Khitma hiyo imeandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kufanyika kwenye viwanja vya maonyesho Nyamazi mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar tarehe 03 Machi, 2024.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Wajane, Ndugu na Jamaa wakati wa khitma ya Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Pili Hayati Ali Hassan Mwinyi aliyefariki tarehe 29 Februari 2024. Khitma hiyo imeandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kufanyika kwenye viwanja vya maonyesho Nyamazi mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar tarehe 03 Machi, 2024.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza wakati wa  khitma ya Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Pili Hayati Ali Hassan Mwinyi aliyefariki tarehe 29 Februari 2024. Khitma hiyo imeandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kufanyika kwenye viwanja vya maonyesho Nyamazi mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar tarehe 03 Machi, 2024.

Watoto wa Madrasa katika khitma ya Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Pili Hayati Ali Hassan Mwinyi aliyefariki tarehe 29 Februari 2024, Khitma hiyo imefanyia katika viwanja vya maonyesho Nyamazi mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar tarehe 03 Machi, 2024.
Baadhi ya Viongozi na Wananchi wakiwa kwenye khitma ya ya Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Pili Hayati Ali Hassan Mwinyi aliyefariki tarehe 29 Februari 2024, khitma hiyo imefanyika katika viwanja vya maonyesho Nyamazi mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar tarehe 03 Machi, 2024.

@ikulu_habari 
@dr.hmwinyi 
@ikulu_mawasiliano 
@samia_suluhu_hassan


Post a Comment

0 Comments