LAAC YAAGIZA UJENZI WA SEKONDARI YA WASICHANA MKOA WA SHINYANGA IKAMILIKE

 
Na Angela Msimbira, SHINYANGA


KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imeagiza ifikapo Septemba  2024 ujenzi wa miundombinu ya shule ya Sekondari ya Wasichana ya 

Mkoa wa Shinyanga uwe umekamilika.


Agizo hilo limetolewa na Makamu Mweyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Staslaus Mabula wakati akikagua mradi wa ujenzi wa shule hiyo katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga. 


Mhe. Mabula ameitaja miundombinu inayotakiwa kukamilishwa kuwa ni mabweni, bwalo, uboreshaji wa nyumba za walimu na ukamilishaji wa miundombinu ya kuvunia maji ya mvua na ufungaji wa gata.


Aidha, Kamati imeridhishwa na usimamizi wa ujenzi wa shule hiyo ambayo hadi kukamilika kwake itagharimu kiasi cha shilingi  bilioni 4.3


Akizungumzia  ukaguzi uliofanywa katika mradi wa ujenzi wa soko kuu, Mhe. Mabula amesema Kamati imeiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kuwa na andiko la mradi linaloanisha gharama zitakazotumika kukamilisha mradi wote pamoja na makusanyo ya  mwezi na mwaka.


Kamati ya LAAC imefanya ziara katika mikoa ya Kagera, Geita, Simiyu, Mara na Sinyanga kwa lengo la kukagua miradi  ya maendeleo 23 inayotekelezwa katika halmashauri 12.


Post a Comment

0 Comments