LAAC YASHAURI USAJILI WA HOSPITALI YA WILAYA BUKOBA UKAMILIKE

 
Angela Msimbira, KAGERA


Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali  za Mitaa (LAAC) imeitaka Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kukamilisha utaratibu wa kupandishwa hadhi Zahanati ya Nshambya kuwa Hospitali ya Wilaya.


Maelekezo hayo yametolewa leo Machi 18,2024 na  Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.  Staslaus Mabula alipokuwa akifanya majumuisho ya ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa  katika Halmashauri hiyo.


Amesema Kamati imesikitishwa na ucheleweshaji wa upandishwaji hadhi ya zahanati hiyo tangu Mwaka 2021 licha serikali kujenga majengo sita ya kuongeza hadhi ya kuwa Hospitali.


"Inasikitisha sana kuona  Halmashauri ya Manispaa ya bukoba  hakuna watu wenye uchungu wa fedha zinazotolewa na serikali ambapo majengo yamejengwa 6 lakini linalotumika ni jengo la wagojwa waa nje tusuala hili halikubaliki hakikisheni hospitali hii inapata usajili na kitumike kama ilivyokusudiwa na Serikali, majengo yanatumika kwa matumizi yasiyokusudiwa  kwa kuwa kwa sasa wanatoa huduma ngazi ya Zahanati wakati majengo yaliyopo ni ya Hospitali ya Wilaya,"amesema.


Aidha, amesema Kamati hiyo ina jukumu la kusimamia matumizi ya fedha za serikali za mitaa nchini hivyo wanakagua fedha zote zinazotolewa na serikali ili kuhakikidha zinatumika kwenye malengo yaliyokusudiwa  na thamani halisi ya fedha ionekane.


Post a Comment

0 Comments