LUIS DIAZ HAJAKATAA TAMAA KUHAMIA LA LIGA

 


Mshambulizi wa Liverpool Luis Diaz, 27, hajakata tamaa ya kuhamia moja ya vilabu vikubwa vya Uhispania La Liga siku zijazo, kulingana na babake mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia. (Daily Mail)

Chelsea ni miongoni mwa vilabu vinavyomhitaji mlinda lango wa Athletico Paranaense Bento, 24, ambaye alicheza mechi yake ya kwanza Brazil dhidi ya England wiki iliyopita. (Globo - kwa Kireno)

Tottenham wanataka kumsajili mshambuliaji wa Feyenoord wa Mexico Santiago Gimenez, 22, kama mbadala wao wa Harry Kane msimu huu wa joto - mwaka mmoja baada ya mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 30 kuondoka kwenda Bayern Munich(Caught Offside)

Manchester United wana nia ya kumsajili beki wa Argentina Aaron Anselmino, 18, kutoka Boca Juniors . (Ole - kwa Kihispania)

Post a Comment

0 Comments