MAN UTD TAYARI ISHAMLENGA MRITHI WA TEN HAG

 


Manchester United wanalenga meneja wa Brentford Thomas Frank kuchukua mikoba ya Erik ten Hag huko Old Trafford msimu wa joto, na sio kocha wa Uingereza Gareth Southgate (Football Transfers)

Hata hivyo, kwa mujibu wa ripoti nyingine mmiliki mwenza Sir Jim Ratcliffe na Ineos wanapanga Ten Hag kuinoa United msimu ujao, lakini wanatengeneza mkakati wa kuweza kusonga mbele haraka iwapo wataamua kuiziba nafasi yake (inews)

Tottenham wana nia ya kukamilisha mkataba wa kudumu kwa mshambuliaji wa RB Leipzig na Ujerumani Timo Werner, 28, lakini wanaripotiwa kuwa hawana haraka ya kuanzisha kipengele cha kumnunua kwa pauni milioni 14.5(Four Four Two)

Arsenal wamefikia ofa ya £51m pamoja na bonasi ambayo Chelsea wametoa kwa Sporting Lisbon kwa mlinzi wa Ivory Coast Ousmane Diomande, 20. (Record kupitia Sun)


Post a Comment

0 Comments