NCHI ZA AFRIKA ZAPEWA USHAURI HUU,BENK YA KCB YATOA NENO.

 


Na mwandishi wetu


IMEELEZWA kuwa Nchi za Afrika, zimetakiwa kuchukua hatua madhubuti za utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti ili kuepuka madhara yanayosababishwa na mabadiliko ya Tabia nchi yakiwemo mafuriko yanayoharibu kingo za mito na kusababisha mmomonyoko wa ardhi.


Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa  Baraza la Taifa la uhifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC) Dkt. Immaculate Semesi katika pori la Pugu Kazimzumbwi Kisarawe mkoani Pwani wakati wa kupanda miti 300 ikiwa ni siku ya mazingira Afrika na Maadhimisho ya Siku ya Prof.Wangari Maathai raia wa kenya mwanaharakati wa mazingira aliyepewa tuzo ya nobel mwaka 1977 kutokana na juhudi za kuhifadhi na kulinda mazingira.


"Lazima tuhakikishe kwamba mazingira  yetu yapo hai, yapo safi, tunadili na masuala ya mabadiliko ya Tabia nchi, tunaishi na ishu za kutokewa  na jangwa, hali hii ikiwa inaendelea hivi, tutashindwa kuishi kwasababu mti ni uhai "


Kwa upande wake, Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Isaac Njenga alisema Kila mmoja ana jukumu kubwa la kuhakikisha kwamba anatunza mazingira kwaajili ya kizazi kijacho 


Naye Naibu kamishna wa hifadhi kutoka TFS Caroline Malunde alisema miti iliyopandwa ni pamoja na migunga na mkangazi ambayo inaoteshwa pembezoni na mito na inastahimili ukame.


Malunde aliwakaribisha watalii wota katika  eneo la kizimzumbwi kwaajili ya kwenda kufanya utalii mbalimbali.


Mkuu wa wateja binafsi na Biashara wa Benki ya KCB, Abdul Juma- alisema wao kama KCB wanaendeleza juhudi za utunzaji mazingira kwa kupanda miti kila mwaka.


Sisi ni wadau wakubwa sana kwenye sekta kwasababu sisi tuna mkakati ambao unaenda kwenye kutunza mazingira ya nchi, huwa tunaweka programu za kupanda miti kwenye kila mwaka" Alisema

Post a Comment

0 Comments