RAIS DKT MWINYI AMEJUMUIKA NA WANANCHI PAMOJA NA VIONGOZI MBALIMBALI KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA HAYATI MWINYI

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amejumuika na Wananchi, Viongozi mbalimbali wa Kitaifa akiwemo Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila, Makamu Mwenyekiti CCM (Bara) Ndugu Abdulrahman Kinana, Mama Mariam Mwinyi na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam kuaga Mwili wa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi. 


Shughuli hiyo ya kuaga mwili imehudhuriwa pia na Mabalozi wanaowakisha nchi zao Tanzania, Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Viongozi wa Dini. 


Mzee Mwinyi amefariki dunia jana tarehe: 29 Februari 2024 katika hospitali ya Mzena, Kijitonyama, Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.


Post a Comment

0 Comments