RAIS DKT SAMIA AWAONGOZA WAOMBELEZAJI WA HAYATI MWINYI UWANJA WA NEW AMAAN COMPLEX

 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amejumuika na Wananchi, Viongozi mbalimbali wa Kitaifa akiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla maalumu ya Mazishi ya Rais Mstaafu wa Zanzibar  na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mzee Ali Hassan Mwinyi  katika Uwanja  wa Amaan, Mjini Magharibi Unguja.


Viongozi wengine ni pamoja na Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Othman Masoud , Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Rais Mstaafu wa Zanzibar Awamu ya Saba Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein na Rais Mstafu wa Jakaya Mrisho kikwete.


Marehemu Mzee Ali Hassan Mwinyi amefariki dunia tarehe: 29 Februari 2024 katika hospitali ya Mzena, Dar es Salaam alipokuwa akipata matibabu na kuzikwa leo Machi 02,2024 Mangapwani Kaskazini Unguja.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa pamoja na Viongozi mbalimbali katika uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar kwa ajili ya kuongoza Viongozi na Wananchi wa Zanzibar kutoa Heshima za mwisho kwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyefariki dunia tarehe 29 Februari 2024 katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa akipata matibabu ya  Saratani ya Mapafu, ambapo anatarajiwa kuzikwa Kijijini kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe 02 Machi 2024.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Makamu wa Rais wa Namibia Mhe. Netumbo Nandi - Ndaitwah alipowasili katika uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar kwa ajili ya kuongoza Viongozi na Wananchi wa Zanzibar kutoa Heshima za mwisho kwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyefariki dunia tarehe 29 Februari 2024 katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es salaam alipokuwa akipata matibabu ya Saratani ya Mapafu, ambapo anatarajiwa kuzikwa Kijijini kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe 02 Machi 2024.Wajane wa Hayati Rais Mstaafu awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi Bibi Siti Mwinyi na Khadija Mwinyi wakiwasili katika Uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar  tarehe 02 Machi 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akizungumza wakati wa kuaga Mwili wa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi katika uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar tarehe 02 Machi 2024

Makamu wa Rais wa Namibia Mhe. Netumbo Nandi  Ndaitwah akizungumza na waombolezaji wakati wa kuaga Mwili wa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi katika uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar tarehe 02 Machi 2024.

Post a Comment

0 Comments