RAIS WA UMOJA WA MABUNGE DUNIANI DKT TULIA ACKSON AWASILI GENEVE NCHINI USWISI

 


Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 18 Machi, 2024 amewasili Geneva nchini Uswisi ambapo amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini humo Mhe. Dkt. Abdallah Possi.


Dkt. Tulia anatarajia kushiriki Mkutano wa 148 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) utakaofanyika nchini humo kuanzia 20 - 28 Machi, 2024.

Post a Comment

0 Comments