RC CHALAMILA AFUNGA BONANZA LA KUPINGA RUSHWA UWANJA WA JK YOUTH PARK

 


Na mwandishi wetu


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Machi 22,2024 amefunga bonanza la kupinga rushwa kwa wanafunzi wa shule za Sekondari katika uwanja wa JK Youth Park Manazimmoja Jijini Dar es Salaam


RC Chalamila amesema moja ya ugonjwa mkubwa unaolikabili bara la Africa ni Rushwa iliyokithiri, ni Rushwa ambayo inazagaa kutoka watu wa kawaida hadi viongozi wa umma wailiopewa dhamana.


Aidha RC Chalamila amesema Club za kupinga rushwa zimewekwa katika mashule kwa lengo la kuelimisha vijana kutambua mapema madhara ya rushwa katika ustawi wa jamii hivyo kinachofanyika leo TAKUKURU wamezikusanya pamoja club hizo kupitia bonanza la michezo kwa lengo la kuendelea kutoa elimu ya kupinga rushwa lakini pia kujenga utambuzi kwa vijana wangali wadogo ili wakifikia umri wa uongozi wasiwe sehemu ya kutoa au kupokea rushwa.


Sambamba na hilo RC Chalamila ametoa zawadi mbalimbali kwa washindi wa bonanza hilo ambao wameibuka na ushindi kupitia mtanange huo vilevile ameahidi kufanya ziara katika shule za Sekondari ili kuweza kutoa elimu zaidi pia kujionea hali halisi ya mazingira ya ujifuzaji na ufundishaji.Post a Comment

0 Comments