TAASISI YA MAMA ONGEA NA MWANAO KUADHIMISHA MIAKA 3 YA RAIS SAMIA MADARAKANI KWA KUFANYA TAMASHA KUBWA

 


Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao inatarajia kufanya Tamasha kubwa kwa watu wenye ulemavu kwa lengo la kusilikiza changamoto zao na kuwapatia mahitaji muhimu ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Steven maelegere maarufu kama (steve Nyerere) alisema tamasha hilo lenye kauli mbiu ya "Mtonye Mwenzako Mama Tena" ambalo litafanyika nchi nzima na kuwaleta pamoja watu wa makundi mbalimbali ikiwemo vijana, mabodaboda, wajasiriamali. 

Alisema taasisi hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan hususani wakisaidia makundi mbalimbali hasa wenye mahitaji maalum. 

"Katika miaka mitatu ya Rais Dkt Samia amefanya kazi kwa vitendo katika kuwahudumia wananchi ikiwemo umeme, sisi kama Taasisi tunawaahidi tutaendelea kuwashika mkondo nyinyi ni wapiga kura nchi hii, nyinyi ni watu kama watu wengine na mnahaki sawa na wengine".

Aidha, amesema Rais Samia amekuwa akijikita katika kusaidia watanzania wa hali ya chini katika kipindi cha miaka mitatu yake ya uongozi anastahili kupongezwa, ameona tatizo la umeme na kulitafutia ufumbuzi na kujenga bwawa la mwalimu nyerere ambalo likianza kutoa huduma tutauza umeme mpaka nje ya Tanzania".

Hata hivyo, amesema pia kwenye sekta ya michezo Tanzania inafanya vizuri imeacha kuwa mtazamaji na mshiriki bali sasa imekuwa mshindani mkubwa na hata kushinda kwenye majukwaa makubwa ambapo wanamichezo wa sarakasi Ramadhani brothers na wengi wengi.

"Na sisi kutokana na jitihada za mama anazozifanya katika kuketa maendeleo katika taifa hili tukajitwika jukumu la kuwavika viatu watoto wa shule ambao hawana uwezo sasa hivi tumebakisha mikoa 13 kukamilisha mikoa yote Tanzania.

Aidha Steve Nyerere amekemea wanaharajati wanaotumia Mitandao ya kijamii kutukana viongozi wa juu Serikalini na kubeza jitihada zao na kuwasisitiza kuwa watumie hoja kupinga na si kutumia matusi katika kukosoa kwao.

Kwa upande wake, Susan Lewis maarufu kama Mama Natasha amesema Taasisi ya Mama ongea na Mwanao inasimamia wasanii mbalimbali ambao wanalenga kutumia Taasisi hiyo kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali ikiwemo kusaidia vifaa vya shule vua watoto na kadhalika.

Nae, Katibu wa Jumuiya ya watu wenye ulemavu ameipongeza Taasisi hiyo kwa kuwashurikisha mara kwa mara watu wenye ulemavu katika shughuli zake mbalimbali ikiwemo makongamano, mikutano na warsha ikiwa ni pamoja na kuwapa misaada watu wenye ulemavu.

"Wanayotafanya mama ongea na mwanao ni kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu katika adhima yake ya kuwainua watu wasiojiweza, wenye ulemavu,wajasiliamali .

Post a Comment

0 Comments