TANZANIA,KENYA ZAKUBALIANA KUONDOA VIKWAZO VYA KIBIASHARA VISIVYO VYA KIUSHURU

 


KUTOKA NCHINI KENYA.


Tanzania na Kenya zimekubaliana na kutia saini makubaliano ya kuondoa vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru ili kuruhusu raia kutoka nchi hizo kufanya biashara baina yao kwa urahisi na kwa manufaa ya pande zote mbili.  


Makubaliano hayo yametiwa saini na Wakili Stephen Byabato Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa na mwenzake Mhe. Rebbecca Miano, Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda kutoka nchini Kenya. Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa Mkutano wa nane (8) wa Kamati ya Pamoja ya Biashara baina ya Tanzania na Kenya katika ngazi ya Mawaziri uliofanyika Kisumu nchini Kenya tarehe 22/03/2024. 


Mkutano huo ulianza kwa ngazi ya watalaam kisha ngazi ya Makatibu Wakuu ambapo zaidi ya vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru zaidi ya 14 vilijadiliwa na kuwekewa mpango wa kuendelea kuviondoa vyote.


Tanzania na Kenya ni wabia wakubwa wa biashara na hivyo kuondolewa kwa vikwazo hivyo vitasaidia kuongezeka mara dufu kiwango cha kufanyika kwa biashara baina ya mataifa hayo.


kulia aliyekaa ni Waziri wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Kikanda wa Kenya Mhe. Peninah Malonza, waliosimama nyuma yao ni Makatibu Wakuu wanaohusika na masuala ya uwekezaji, viwanda, biashara na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi wa Tanzania nchini Kenya na Balozi wa Kenya nchini Tanzania.Post a Comment

0 Comments