TCAA YASEMA TANZANIA IPO TAYARI KUJIUNGA NA SOKO LA PAMOJA,JOHARI AITAJA ATCL.

 


Na mwandishi wetu

MAMLAKA ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA) limesema kwa sasa taifa lipo teyari kujiunga na soko la pamoja la ndege Afrika na kusema soko hili linafaida kubwa kwa mashirika ya ndege nchni.


Faida hizo ni kuongezeka kwa masoko ya ndege nchini kutokana na ndege hizo kwenda kwenye anga mbalimbali bila kikwazo chochote,mashirika mbalimbali  ya ndege kutua nchini pamoja na kuongezeka kwa kodi nchini.


Haya yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa TCAA,Hamza Johari,wakati wa kikao cha kupata maoni ya namna ya Tanzania inavyoweza kujiunga soko la pamoja.


Aidha,Johari,amesema kwa sasa taifa lipo tayari baada ya kukua kwa mashirika ya ndege nchini.


"Hapo mwanzo tulishindwa kujiunga kwenye soko la pamoja kutokana na mashirika yetu ya ndege yalikuwa bado hajakuwa,ila kwa sasa mashirika yetu yameshakuwa ndio tumeamua kujiunga"Amesema Johari.


Hata hivyo,Johari ametolea mfano shirika la ndege nchîni(ATCL) limeshakuwa kubwa sana kutokana na kuwepo ndege za kisasa.


"Kiukweli naimani sana na shirika la ATCL sahivi lina ndege zaidi ya 14,na dhumuni letu ni kuhakikisha Abilia anaweza kusafiri kwa urahisi."Ameongeza kusema.


Kwa Upande mwalimu wa Chuo cha usafirishaji nchini(NIT),Juma Fimbo,amesema mbali na Taifa kupata manufaa makubwa kutokana na kujiunga na soko la pamoja pia itafungua milango na mashirika makubwa ya kimataifa ya ndege kutua nchini.

Post a Comment

0 Comments