TETESI ZA SOKA ULAYA LEO IJUMAA MARCH 08,2024

 


Thomas Tuchel amelenga kurejea kama kocha wa Chelsea atakapoondoka Bayern Munich majira ya joto, lakini kocha huyo wa Ujerumani pia anavutiwa na Manchester United na Barcelona. (Sky Sports)

Wamiliki wa Liverpool walikutana na Michael Edwards Jumapili katika majaribio yao ya kumshawishi mkurugenzi wa zamani wa michezo wa klabu hiyo kuunda nafasi mpya baada ya Jurgen Klopp huko Anfield. (Mail)

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta anasema kiwango cha kuvutia cha timu yake mbele ya lango hakitabadilisha mipango ya klabu hiyo ya uhamisho, huku The Gunners bado wakitarajiwa kusajili mshambuliaji katika majira ya joto. (ESPN)

Mlinzi wa kushoto wa Arsenal Oleksandr Zinchenko analengwa na Newcastle United na Bayern Munich, huku The Gunners wakitaka euro 38.5m (£32.9m) kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ukraine, 27. (Football Transfers)


Wakala wa winga wa Georgia Khvicha Kvaratskhelia anasema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ataondoka Napoli ikiwa klabu hiyo ya Italia itapokea ofa ambayo haiwezi kukataa. (Gazzetta dello Sport )

Mabosi wa Manchester United wanatarajiwa kumzuia Mason Greenwood kwenda Marekani kwa ziara ya kujiandaa na msimu mpya baada ya mshambuliaji huyo wa Uingereza, 22, kurejea kutoka Getafe alikokuwa kwa mkopo. (Star)

Greenwood yumo kwenye orodha ya wachezaji wanaoweza kusajiliwa na Barcelona, ambao tayari wameshapiga hatua kuelekea mkataba wa bei nafuu msimu huu wa joto. (Sport )

Post a Comment

0 Comments