TETESI ZA SOKA ULAYA LEO IJUMAA MARCH 15,2024

 


Chelsea wanahofia kuwa watamkosa mchezaji wa Napoli, Victor Osimhen, 25, katika uhamisho wa majira ya joto, huku Paris St-Germain na Arsenal zikiongeza juhudi katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji huyo mahiri wa timu ya taifa ya Nigeria. (Teamtalk).

Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, 26, hatarajiwi kuhamia PSG msimu huu wa joto kufuatia ripoti kwamba Muingereza huyo atachukua nafasi ya mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 25. (Sky Sports).

Getafe hawataweza kuwa na Mason Greenwood zaidi ya muda wake wa mkopo kwani Manchester United wameamua kumuuza mshambulijai huyo wa Uingereza, mwenye umri wa miaka 22. (Marca kwa Kihispania)

Manchester City wameamua kuahirisha mazungumzo ya kumpa mkataba mpya kiungo wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, 32, ambaye amebakiza zaidi ya mwaka mmoja katika mkataba wake wa sasa. (Football Insider)


Aston Villa wana imani kuwa wataweza kumbakisha kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz licha ya kumtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kutoka Arsenal. (90 Min)

Meneja wa England Gareth Southgate amefichua kuwa amekiambia Chama cha Soka kufanya mazungumzo kuhusu mustakabali wake hadi baada ya Euro 2024. (Mirror).

Mchezaji wa zamani wa Manchester City na kocha wa sasa wa Saudi Arabia Roberto Mancini analengwa na Newcastle United iwapo wataamua kuchukua nafasi ya Eddie Howe msimu huu wa joto. (HITC)

Newcastle wanataka kuharakisha kuondoka kwa Dan Ashworth kwenda Manchester United huku mkurugenzi wa michezo wa Monaco Paul Mitchell akiongoza orodha fupi ya wagombea kuchukua nafasi yake. (Telegraph - usajili unahitajika)

Post a Comment

0 Comments