WAKULIMA NJOMBE WAMSHUKURU RAIS SAMIA

 Na mwandishi wetu

Wakulima wanaolima Nyanya Mkoani Njombe wamemshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuboresha Mazingira ya Upatikanaji wa mbolea na soko la uhakika la mazao yao.

Shukrani hizo zimetolewa na wakulima hao waliokutwa na Mhe Kissa Gwakisa Kasongwa , DC wa Njombe wakati wakiwa wanachambua nyanya pembezoni mwa barabara.

Ikumbukwe kuwa  Njombe ni moja ya mikoa inayoongoza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula nchini,  hivyo kilimo ni maisha ya kila siku ya wananchi wa Mkoa huo 

Mhe  Kissa alipowauliza wakulima kama wana changamoto, wakulima hao walisema hawana changamoto bali wanaomba serikali iendelee kuboresha masoko zaidi.

 

Post a Comment

0 Comments