WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHI.

 Na mwandishi wetu

WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa leo Machi 22, 2022 amezindua ripoti ya Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ya Vijiji Wilayani Ruangwa mkoni Lindi, uzinduzi ambao umeenda sambamba na utoaji wa vyeti 18 vya ardhi ya Kijiji.


Waziri Mkuu amefanya uzinduzi huo katika Mkutano wa Wadau Kujadili Utekelezaji Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi, uliohusisha wadau mbalimbali wa masuala ya ardhi kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya ruangwa.


Waziri Mkuu ameeleza kuwa Lengo la Serikali ni kupima ardhi yote nchini ili wananchi wakiwepo wanavijiji waweze kuitumia katika kufanya shughuli za kiuchumi.


Amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi ambao Halmashauri zao zinafikiwa na mradi kuhakikisha kuwa wanashirikiana na Wizara ya Ardhi katika kufanikisha mradi huo.


“Nisisitiza Wakuu  wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wenyeviti na Watendaji katika vijiji washiriki kikamilifu kuwafikia wananchi na kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa matumizi sahihi ya ardhi, ili waweze kunufaika pamoja na kupata hati milki za ardhi wanayoimiliki”


Waziri Mkuu pia amesema juhuhudi zinazofanyika katika upimaji wa ardhi nchini ni matokeo ya utendaji kazi na usimamizi mzuri unaofanywa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.


“Mhe. Rais amekuwa mstari wa mbele katika kusisitiza juu ya upimaji wa ardhi, hata nilipomuambia nakuja huku amenipa salamu zenu na anafuatilia hiki kinachondelea kupitia vyombo mbalimbali vya habari na Serikali yake itaendelea kutenga bajeti kwaajili ya kazi ya upimaji”


Awali, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda, alisema mradi huo utavifikia vijiji vyote katika wilaya ya Ruangwa, ili kuhakikisha kuwa mpango wa matumizi bora vijijini unapata mafanikio makubwa.


Post a Comment

0 Comments