WEMA SEPETU AULA DILI YA UBALOZI HELABET

 


Na mwandishi wetu

Kampuni ya michezo wa kubashiri ya Hela bet imempa Msanii wa filamu Tanzania Wema Isack Sepetu Ubalozi  kwenye kampuni hiyo ambayo inaendesha michezo huo mtandaoni.

Akizungumza leo Jijini wakati akipewa Ubalozi huo amesema kuwa amefurahi kuwa mwanafamilia mpya kutoka kwenye namba moja ya kampuni ya kubashiri ya michezo.

Wema amesema kuwa baada ya kuitathimini na kujiridhisha kuwa kampuni ipo vizuri ameamua kuwa balozi wake na ataendelea kujifunza na kutoa elimu kwa wananchi.


“Mimi huwaga sifanyi  na kampuni ambayo haiko vizuri lakini kwa kuona hii kampuni ya hela bet inafanya vizuri kwa upande wa michezo mtandaoni nikaona nishirikiane nao ili tuweze kufanya kazi.


Hata hivyo ameahidi kufanya kazi bega kwa bega kwa kampuni hii ili kuhakikisha inamfikia kila Mtanzania na pia mimi  nitaanza kubashiri na kwa upande wa timu mimi ni shabiki wa Yanga.

Post a Comment

0 Comments