ATHARI ZA TABIANCHI BADO NI TATIZO,WANAHABARI WATAKIWA KUPAZA SAUTI.

 


Na mwandishi wetu


IMEELEZWA kuwa kama jitihada za makusudi zisipofanyika katika kudhibiti vitendo vya ukataji wa miti na ujengaji holela kwenye vyanzo vya maji basi jamii ijiandae kukutana na mabadiliko ya Tabianchi ikiwemo kutokea na Mafuriko na Joto kali.


Rai hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Ringo Mowo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi isiyo ya kiserikali inajihusisha na masuala mazima ya hali ya  mazingira ya Sharon Ringo Foundation wakati wa  kupitia warsha ya waandishi wa habari juu ya mafunzo juu ya uelewa wa mabadiliko tabianchi kupitia mradi unaoendeshwa na Sharon Ringo Foundation kupitia udhamini wa Plan International Tanzania. Mkufunzi mbobezi, Henry Kazula kuzungumzia athari za mabadiliko ya tabia nchi.


"Jamii isipochukua hatua za haraka huku tunapokwenda ni kubaya ikiwemo kwa watoto wetu,tumeona wenyewe hapa nchini kuna maeneo mbalimbali yamekubwa na mafuriko ,joto kupita kiasi hata ukame pia yote yanatokea kutokana na hizi athari za mabadiliko ya Tabia Nchi"Amesema Mowo


Hata hivyo,Mkurugenzi  amezitaka jamii za kitanzania iwe mwanasiasa,mwananchi wa kawaida,viongozi wa dini kuamka kwa ajili ya kupambana na athari hizi za Mabadiliko.


"Tunavyosema kila mmoja wetu amke kupambana na hili kwani Mafuriko hayachagui mtu wa aina yeyote na kila mtu ajitokeze kwenye hili"


Aidha,Mowo, amesema jamii iwetakiwa kuwa na mkakati wa haraka wa kuwepo kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwajengea tabia ya watoto kupenda kupanda miti pindi wakiwa hata shuleni kuweza kusaidia.


Sanjari na hayo pia,Mowo,amewataka wanahabari pamoja na asasi mbalimbali kuzidisha utoaji Elimu ili watu wawe na uelewa juu ya suala nzima ya athari za mabadiliko ya tabianchi.


"Nyinyi kama wanahabari na jamii kwa ujumla kuzidisha kutoa elimu pia mbali na kufikisha elimu kila mmoja wenu ajipange kutika kupambana na athari zozote za Mabadiliko ya Tabianchi."

Post a Comment

0 Comments