BASHUNGWA AWASILI MANYARA, KUSHUHUDIA UTIAJI SAINI MKATABA WA UJENZI BARABARA.

 Na mwandishi wetu,Manyara

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa (Mb) amewasili Wilayani Babati Mkoani Manyara ambapo atashuhudia utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa barabara ya Dareda - Dongobesh (km 60), Sehemu ya Dareda Centre hadi Dareda Mission (km 7) kwa kiwango cha lami.

Bashungwa amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge Babati Vijijini, Daniel Sillo, leo tarehe 06 Aprili 2024.Post a Comment

0 Comments