BERNARDO SILVA ANATAKA KUHAMIA BARCELONA

 


Mshambuliaji wa Ureno Joao Felix anasema mchezaji mwenzake wa kimataifa Bernardo Silva, 29, anataka kuhamia Barcelona, ​​huku kiungo huyo wa kati wa Manchester City akihusishwa na klabu hiyo ya Catalan mara kadhaa hivi majuzi. (Gerard Romero)

Liverpool wameanza mazungumzo na mkufunzi wa Sporting Lisbon Ruben Amorim, 39, kuchukua nafasi ya Jurgen Klopp huko Anfield. (Foot Mercato - kwa Kifaransa)

Barcelona pia walikuwa wanamtaka kocha huyo wa Ureno lakini wamesitisha mpango huo kwani wanafikiri huenda akaelekea Liverpool. (Sport - kwa Kihispania)

Manchester United wanafikiria kumnunua mlinzi wa Aston Villa wa Uingereza Ezri Konsa, 26. (Footbal Transfers)

Post a Comment

0 Comments