BIL.27 KUKARABATI HOSPITALI KONGWE 31

 
SERIKALI katika mwaka wa fedha 2022/23 imetoa Sh Bilioni 16.5 kwa ajili ya ukarabati wa Hospitali kongwe 19 ambapo kwenye mwaka wa fedha 2023/24 kiasi cha Sh Bilioni 27.9 kilitengwa kukarabati hospitali kongwe 31 zilzobaki ikiwemo Hospitali ya Magunga katika Halmashauri ya Mji wa Kongwe ambayo imetengewa Sh Milioni 900. 


Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Dkt Festo Dugange alipokua akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini, Mhe Dkt. Alfred Kimea aliyehoji ni lini Serikali itafanya ukarabati mkubwa wa Hospitali kongwe ya Magunga Korogwe.

Post a Comment

0 Comments