CHELSEA YATOA MACHO KWA BRUNO FERNANDES NA RASHFORD

 


Chelsea inapaswa kuwavutia kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes, 29, na mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 26, kuondoka Manchester United msimu huu wa joto, kulingana na mlinzi wa zamani wa Blues William Gallas (Mirror)

Chelsea hawana nia ya kumsajili mlinda lango wa Athletico Paranaense Bento, 24, lakini Inter Milan wanatazamiwa kukabiliwa na ushindani kutoka kwingineko kwenye Ligi ya Premia kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil. (Gazetto dello Sport - kwa Kiitaliano)

Borussia Dortmund wana nia ya kumsajili winga wa PSV Eindhoven Johan Bakayoko, 20 . Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji pia anaripotiwa kulengwa na Burnley na Brentford . (Voetbal International - kwa Kiholanzi)

Beki wa Everton na England Jarrad Branthwaite anasema anazuia kelele kuhusu mustakabali wake huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 akivutia Manchester United na Real Madrid .(90min)

Post a Comment

0 Comments