DC RORYA ADAIWA KUKWAMISHA JITIHADA ZA WADAU WA ELIMU

 Na mwandishi wetu,Rorya


Mjumbe  wa Mkutano Mkuu Taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Sango Kasera Gungu ambaye pia ni mdau wa maendeleo katika Wilaya ya Rorya Mkoani Mara amedai kushindwa kuendelea na mpango wa ugawaji wa madawati kwenye shule 132 ambazo zimekuwa na changamoto ya uhaba wa madawati kutokana na zoezi hilo kuzuiliwa na Mkuu wa Wilaya hiyo akishirikiana na Mwenyekiti wa CCM Wilayani humo.


 Akizungumza wakati wa zoezi hilo kusitishwa na kukosa ushirikiano kutoka kwa watendaji,Sango amedai kushangazwa na kitendo hicho kutokana na kwamba jambo ambalo alikuwa analifanya ni msaada wa kunusuru watoto kukaa chini pamoja na kusapoti jitihada za Mhe,Rais Samia Suluhu Hassan za kuwajenga mazingira Bora ya kujifunzia wanafunzi.


“Ni kwamba zoezi hili tumeanza mwezi mmoja uliopita tumezingatia kwa kufuata taratibu zote kwa kuandika Barua ,kwa Mkuu wa Wilaya,Katibu wa CCM Wilaya ya Rorya na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rorya na Mwenyekiti wa Chama lakini nimesikitika siku ya Jana Mhe,Mkuu wa wilaya alinipigia simu na kuniambia zoezi la kugawa nilisimamishe kwani majukumu ya kuleta maendeleo ni ya serikali na sisi tulikuwa tunafanya kwa nia nzuri tu kwasababu tunaamini maendeleo yanaletwa na sisi wanarorya na mimi sijafanya peke yangu ninamarafiki zangu wanafanya kazi zao kwenye wilaya ya rorya ni wachina wamekuwa wakiniunga mkono kwa kutoa vitu awatoi fedha”Sango Kasera Gungu Mjumbe  wa Mkutano Mkuu Taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM)


Aidha ameongeza kuwa awali zoezi hilo lilizinduliwa na Mkuu wa wilaya ya Rorya Juma Chikoka ambaye alitoa ridhaa ya kumruhusu  kuendelea na shughuli nzima ya ugawaji lakini hatima ya mwisho baada ya kugawa kata mbili ndipo alipigiwa simu ya kukatazwa kwa madai yawezekana akawa anajipalilia kupata ubunge mwaka 2025.


“Ninaomba kumuondoa wasi wasi Mkuu wa wilaya na Mwenyekiti wangu wa chama mimi sitoi msaada kwa kujionesha au kwa kutaka kitu furani kama wao wamekuwa wakidhani nataka ubunge sina mpango wa ubunge wala udiwani ninachofanya ni kuwasaidia wadogo zetu ambao wapo shuleni na wala sio kutafuta madaraka au sifa yoyote hile kwenye jamii yangu” Sango Kasera Gungu Mjumbe  wa Mkutano Mkuu Taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM)


“Nasikitika Pia hata Mwenyekiti amekuwa akiwapigia wajumbe na wanachama wa CCM wasije kwenye makabidhiano, nimekabidhi kata ya Chigunga  Mhe mkuu wa wilaya nilimuita na kumuomba awepo akasema hayupo atatuma mwikilishi ambaye ni afisa elimu lakini kilichoendelea nazuiliwa nisikabidhi imenisikitisha sana” Sango Kasera Gungu Mjumbe  wa Mkutano Mkuu Taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM)


 


 


Kufuatia madai haya kumuelekezea Mkuu wa Wilaya hiyo,Mhe Juma Chikoka ,amesema wilaya anayoiongoza aijazuia wadau wa maendeleo kutoa misaada ya kielimu na mingine jambo la msingi ni wao kufuata utaratibu wa kukabidhi misaada ambayo wanaitoa  kwenye mamlaka na sio kwenda kukusanya watu pasipo kufuata utaratibu wa unaotakiwa.


“Kwanza nimpongeze Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa  Sanga Kasera anachokifanya ni jambo zuri na ndicho ambacho serikali inahamasisha na kuwaomba wadau mbali mbali wajitokeze kuongeza nguvu na kuunga jitihada za Mhe Rais za kutaka kuona maendeleo kwenye sekta ya elmu yanakua kwa kasi kubwa,tumepokea misaada mbalimbali ya madawati na vitanda lakini hawa wote wamekuwa wakifuata utaratibu wa kuja na kukabidhi ofisini kwa Mkuu wa wilaya kwa maana ninapopokea mimi na mimi nampatia Mkurugenzi yeye anajua wapi kwenye shida na mwisho wa siku anagawa msaada huo”Juma Chikoka Mkuu wa WIlaya ya Rorya.


“Naomba tu kama kuna mtu anajambo na anataka kutoa msaada naomba sana awasiliane na kukabidhi kwa mkuu wa wilaya na serikali ya Wilaya aijawai kuzuia na aitazuia kamwe misaada ya wadau na wahisani mbalimbali shida iliyopo watu wakiwa watano wakasema wanatoa misaada na kuanza kuzunguka bila utaratibu tunaweza kusababisha shida ya kiusalama jambo la msingi lazima utaratibu ufuatwe na milango ipo wazi wakati wote” Juma Chikoka Mkuu wa WIlaya ya Rorya.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya eya Rorya Ongujoe Wakibara amesema wao jukumu lao ni kusimamia utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi kwa kukagua na kwamba yeye anauwezo wa kumzuia mtu yoyote jambo linalotakiwa ni mtu au taasisi zinazotaka kutoa msaada kufuata taratibu ambazo zimewekwa kwa mujibu wa sheria.


“Mimi nilichokosema kwenye Kikao Juzi Rorya tunamapungufu ya vitu vingi na sisi hatuzui mtu kuleta msaada lakini afuate utaratibu kama analeta kichama alete kwenye chama watapeleka sehemu husika,kama ni kiserikali aende uko kwenye serikali nani anaweza kuzuia msaada usije hayupo anayekataa sisi tunaomba alete msaada lakini afuate utaratibu” Ongujo Wakibara, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Rorya


Post a Comment

0 Comments