DK.MWINYI APOKEA SALAMU ZA POLE KUTOKA KWA RAIS WA SOMALIA

 Na mwandishi wetu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amepokea  salamu za pole kutokana na kifo  cha Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mzee Ali Hassan Mwinyi kutoka kwa Rais wa Shirikisho la  Jamhuri ya Somalia Mhe.Dkt.Hassan Sheikh Mohamud.

Viongozi hao walikutana leo tarehe 28 Aprili 2024 Ikulu , Migombani. 

Mzee Mwinyi alifariki dunia tarehe 29 Februari, 2024 Dar es Salaam na kuzikwa tarehe 02 Machi  2024 kijijini kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Rais Dk.Mwinyi amemshukuru Rais Dkt.Mohamud kwa salamu za mkono wa pole na kuja kuwafariji.


🗓️28 Aprili 2024

📍Ikulu , Migombani.

Post a Comment

0 Comments