DKT BITEKO MGENI RASMI TAMASHA LA MKESHA WA MUUNGANO

 


Na mwandishi wetu

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Doto Biteko Leo 25 Aprili, 2024 ameshiriki kwenye Tamasha la mkesha wa miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika sambamba na maadhimisho ya miaka 10 ya Efm Radio. 


Hafla hiyo inayofanyika kwenye viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam, imevutia mamia ya washiriki kutoka pande mbalimbali za Jiji.


Tamasha pia limehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila, Naibu Mawaziri,  Makatibu Wakuu, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Toba Nguvila, Wakuu wa Wilaya za mkoa wa Dar es Salaam, Msemaji mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi na watendaji wengine wa serikalini.


Watanzania kesho wanaadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Sherehe zitafanyika katika katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Post a Comment

0 Comments