DKT TULIA ACKSON APOKEA TUZO MAALUM KUTOKA WIZARA YA MAJI

 


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzanzua Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amepokea Tuzo maalum ya Siku ya Maji Duniani kutoka kwa Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso kwa kutambua mchango wake na Bunge kwa ujumla katika sekta hiyo tukio lililofanyika leo tarehe 5 Aprili, 2024 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. 


Aidha, Tukio hilo limeshuhudiwa na Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi. Kundo Andrea Mathew, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi. Mwajuma Waziri, Naibu Katibu Mkuu Bi.Agnes Meena pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, Mhe. Jackson Kiswaga.


Tuzo hizo hutolewa tarehe 22 Machi kila Mwaka katika maadhimisho ya siku ya Maji Duniani.Post a Comment

0 Comments